NAHISI NINA MIMBA YAKO
Muda wote Henry alikua ni mtu mwenye furaha na anatabasamu lakini baada ya kupokea ujumbe mfupi kutoka kwa catty tabasamu likatoweka usoni.Basi Kwasababu ilikua ni chakula Cha pamoja kwa familia kulikua na stori nyingi za hapa na pale.
Humphrey hakuelewa kinachoendelea kwa rafiki yake Basi akawa anamtania tu
Humphrey: kwahiyo mwanangu Kama utani unachukua jiko,
Henry: we si unataka uzeeke ngoja watu wazima tukuonyeshe njia ya kupita,
Humphrey:Sema Nini mwanangu nahisi ntawahi kuoa, na tutaongea Kuna suala muhimu mno.
Basi wakatawanyika kila mtu na safari yake, mzee Mkole, Henry pamoja na Humphrey walikua na safar ya kurudi Dar es salaam.wakati baba yake mdogo Henry yeye anaishi mbeya akifanya biashara zake na ni mtu aliefanikiwa katka biashara zake.
Baada ya kuondoka pale walielekea kwa baba ake mdogo Henry ili walale siku hiyo kesho yake waanze safari.Baba ake mkubwa pamoja na shangazi ake Henry ambaye ni aunt Maya wao walisafiri usiku kwa gari yao kuelekea Mafinga.
Giza likaingia baridi ikiwa imekolea kweli na kwa watu waliotoka mazingira yenye joto hata baridi ya mwezi wa tatu kwa mkoani mbeya iliyoambatana na mvua ilikua inawatesa.Henry na Humphrey baada ya kuoga walienda kupumzika. Henry akampigia Simu Nissy "hello"
Nissy: hello hubby
Henry: Tushafika kwa mzee hapa nkaona nikujulishe, Ila nmechoka Sana
Nissy:poleh jaman inabidi upumzike, hata Ivo nlikua nasubiri utulie kidogo ndo nikutafute,
Henry:Mmmh umesubiri mpaka nikutafute na ulikua na la kuniambia! enhe niambie
Nissy: Baby I really thank you, umekua mwanaume mkweli kwangu! Hii n heshima umeileta katika familia yangu,
Henry:usijal nlikwambia Sina mpango wa kukupotezea muda, Yale yote nlokuahidi ntafanya ndo nimeanza
Nissy: kweli nimeamini wewe sio muongo,nakupenda!
Henry: nakupenda piah sana, Sasa nilale mpenzi si unajua kesho natakiwa kuamka mapema Sana.
Nissy: eeeh kweli pumzika, yani we hujui tu nnavotamani asubuh niwahi nikusindikize.
but anyways usiku mwema
Henry:najua, lakini sitaki kumsumbua mke wangu,
Basi wakacheka wakaagana.
.
Kulivokucha wakawahi airport ili kurudi Dar es salaam.Mzee Mkole ni mfanya biashara mkubwa tu jijini Dar na aliishi yeye tu na mwanae Henry, hakukua na mwanafamilia mwingine walieishi nae kwakua Mama ake Henry alikwisha fariki Henry akiwa bado mdogo, Hivyo mzee Mkole hakuoa Tena alimlea tu mwanae akiwa na watu wa kumsaidia kazi nyumbani.Basi walipoingia ndani wakapokelewa vizuri na binti wa pale nyumbani kwao, alizoea kumwita mzee Mkole baba na Henry Kama Kaka ake,
Binti:karibuni baba poleni na safari
mzee Mkole: Asante, habari za hapa nyumbani,
Binti:salama kabisa shkamoo,(Huku akiwapokea mabegi yao)
Mzee Mkole: marhaba, Kuna jipya lolote??
binti;hapana
mzee Mkole: Kama Kuna jipya mtamwambia Henry me ntakua ndani napumzika!
kila mtu akaelekea kwenye chumba chake, ilikua n nyumba kubwa ya ghorofa moja inayopatikana mbezi beach ikiwa na vyumba visivyopungua vitano vya kulala, sebule kubwa pamoja na sehemu ya kupata chakula, nje ikiwa na parking kubwa ya magari, garden pamoja na bwawa la kuogelea(swimming pool). Henry alipofika chumbani kwake akajitupa kitandani na usingizi ukamchukua akashtushwa na Simu ambayo ilikua ikiita, akaitoa Simu mfukoni na kuangalia Catty alikua anapiga.akapokea
Catty: Henry
Henry:nlipata ujumbe wako sema nlikua bize kidogo, enheee nipange
Catty:ndo Kama nlivyokwambia, nimepima inaonyesha ni mjamzito.
Henry:hmm! lakini Catty hakuna kitu kinaendelea kati yetu na wewe unajua, Sasa we unategemea mimi hili suala nalipokeaje?
Catty:najua kwamba ilikua bahati mbaya tu, lakini sikutaka kuficha bado ni damu yako,
Henry:Haya niambie wewe unataka nifañye Nini?
Catty:Aiseee Mimi ndo kwanza natakiwa kurudi chuo hivi kàribuni sijui familià yangu itapokeaje Hili suala...au nitoe?
Henry:Unakichaà? Unàtakakufa? basi imeshakua tutalea kwakua umesema Mimi ndo muhusika,
Catty:Sio rahisi Sana Kama unavochukulia wewe, yule mzee wangu ndo nnaemhofia,
Henry:ntakutafuta tuongee zaidi, (akakata Simu)
akijisemesha mwenyewe "aisee siji Tena kunywa pombe"
Comments
Post a Comment