NDOA YANGU
'NDOA YANGU'
Kulikua na Hali ya hewa ya utulivu kukiwa na kiubaridi kiasi pamoja na mvua ndogo ndogo zinanyesha jijini mbeya majira ya mwezi wa tatu, soko matola ni miongoni mwa maeneo yanayopatikana katikati ya jiji Hilo kukiwa na watu changanyikeni yaani watu wa kabila na dini tofauti tofauti..lakini pia Kuna nyumba nyingi ambazo zilijengwa zamani yaani ni nyumba chakavu.Katikati ya nyumba hizo chakavu ndipo inapatikana nyumba ya mzee Patrick.Katika nyumba ya mzee Patrick kulikua na pilika pilika za hapa na pale maandalizi ya kupokea wageni wanaokuja kuoa katika familia ya mzee Patrick, ilikua ni familia ya kawaida tu ya mke mmoja na watoto wanne.Ikiwa na watoto wa kiume wawili na watoto wa kike wawili yaani Nikki,Bora,Nissy na Shuku.
mama Nikki:Mama fau nakuomba Basi ikifika mida ya saa Saba kila kitu kiwe kimemalizika.
alisikika mama ake Nikki akimwambia mdogo wake ambaye alikuja kwaajili ya kumsaidia dada ake kufanya maandalizi ya kumwozesha binti ake.
mama fau: Dada Wala usijali hakuna kitu kitaharibika
Huku mzee Patrick (baba Nikki) akiwa ndani anazungumza na baadhi ya ndugu zake ambao wamefika pale kupokea mahali.
Nissy akiwa ndani chumbani kwake ambako alikua akizungumza na shangazi zake wakimpa maelekezo na kumfunza jinsi ya kuishi na mume atakapoenda kuishi na huyo mume wake.Wakamweleza mambo mengi mno kiasi kwamba Nissy pamoja na kuwa mtoto wa mjini Sana hakutegemea Kama maneno yale yalikua yanatoka kwa shangazi zake alokua anawaheshimu haswaaa.Akaanza kuona aibu aking'atang'ata midomo huku macho kainamisha chini
shangazi 1:ndo utusikilize vizuri mambo ya kutiana aibu sisi hatutaki, Mara ooooh huyu atakua akufunzwa tusije kusikia.
Shangazi 2:lakini Nissy una hakika huyo mkwe anakuja leo?isijekutokea Kama yaliyotokea mtaan kwetu.
Nissy:aunt buana atakuja, kwani mtaani kwenu kilitokea Nini?
Shangazi 2: binti alikua na hakika kabsa kwamba anakuja kutolewa mahali Sasa ukafika muda kijana hakutokea na walikua wamefanya maandalizi ya kutosha vyakula vimepikwa vya kutosha, saa8,saa 9 mpaka Giza linaanza hakuna wageni aiseee ilikua kituko .
Nissy:weweee aunt usiniogopeshe jamani
enhe kwaiyo wakafanyaje? Kwasababu hata sitamani kuwaza maumivu ya huyo dada
Shangazi 2: wafanye Nini, sema yule mzee alikua kiboko, alimuuliza mwanae kama anakufahamu nyumban kwa huyo kijana yaani kwa wazazi wake kabsaa na kumbe haikua mbali Sana kutoka pale kwake, Basi kabeba gari kapakia vyakula vyote kaenda kuwapelekea na kuwadai wamlipe fidia kwa kupoteza muda pamoja na vyakula vyake, buana walishangaa lakini walilipa maana mzee alikua amefura haswaaa.....
woote wakacheka, Nissy akachukua Simu yake na kuingia katika ukurasa wa kuandika ujumbe mfupi,akaandika "hello mmefika wapi?"
baada tu ya dakika moja akapata ujumbe kupitia Simu yake "soon I will be there don't worry"
Nissy akajibu "Ok"
Nissy:Aunt wamesema watafika sio muda sana
wote(shangazi 1 na 2):afadhali.
MAPOKEZI YA BWANA HARUSI MTARAJIWA
Ni majira ya saa nane za mchana jua likiwa limewaka vizuri na zile mvua ndogo ndogo zimekoma.Gari mbili zinaegeshwa nje ya nyumba ya mzee Patrick ambaye ndo baba mzazi wa Nissy wageni wakashuka kuelekea ndani ya nyumba.
Gari zilizokua zimeegeshwa nje ya nyumba ni gari nzuri kweli ukilinganisha na mazingira yaliyopo maeneo hayo, Basi walikua wameongozana vijana wawili wanaoendana umri yaani Henry pamoja Humphrey pia baba mtu mzima alievalia mavazi mazuri Mr Mkole ambaye ni baba mzazi wa Henry akiwa na umri karibia miaka hamsini na zaidi, akiwa ameambatana na ndugu zake yaani Kaka ake mmoja na wadogo zake wakike mmoja pamoja na wakiume mmoja yaani baba mkubwa, baba mdogo pamoja na shangazi ake Henry piah waliambatana na mzee mwingine ambaye n mwenyeji wa maeneo ya soko matola mzee mashaka akiwa amekuja Kama mshenga wa familia ya Mkole.
ndani Nissy akapokea ujumbe mfupi kupitia Simu yake "tunaelekea getini"
Nissy:aunt wamefika wapo nje
shangazi 1.:anhaaa sawaaa, mambo niyapendayo haya...
wakatoka nje
walipofika getini Kama kawaida ya Mila za kabila lao wakatandika kitenge chini mlangoni afu wakaweka fedha kiasi Cha shilingi elfu hamsini kwenye kitenge. af wao wakasimama pembeni wakiwakaribisha
mshenga ambaye ni mzee mashaka akamwambia Henry hapa ili tuingie ndani tunatakiwa tuweke shilingi elfu hamsini nyingne au zaidi, Henry na Humphrey wakaangaliana usoni wakatabasamu tu, afu Henry akaingiza mkono mfukoni akatoa kiasi Cha shilingi laki moja akitaka kuweka pale kwenye kitenge
shangazi ake Henry ambaye anaitwa Maya
akamdaka mkono Henry
Aunt Maya:mmmmh punguza papara mwanangu humo ndani hata hatujaingia.....(kwa sauti ya chini) akachomoa noti Kama nne hivi kwenye zile hela alizoshika Henry afu ikawekwa shilingi elfu sitini kwenye kitenge, kitenge kikaondolewa wakapita mpaka ndani.walipofika maeneo ya Uani kulikua na majiran Kama wawili ambao walialikwa na mama Nikki ili kuwasaidia kazi pamoja na kuwataarifu wanakijiji wengine kwamba binti ake anaolewa....
jirani 1: atakua n huyo Kaka alienyoa upara,
jirani 2:lakini huyo Kaka mwingine anaonekana ndo muoaji....
walikua wakiambiana wao kwa wao bila kupata majibu kamili, Basi walisalimiwa wakapita mpaka ndani, Kama kawaida kwenye viti pia zikawekwa hela hivyo ili wakae ikabidi waweke hela nyingne mwishoni wakakaa chini ili kuendelea na taratibu nyinginezo.....
familia ya mzee Patrick iliwapokea vizuri wageni wao lakini wao pia walikua na mshenga wao ambae ndie anakua msemaji kwa upande wao.
Mshenga: karibun Sana pia poleni na safari, lakini kabla hatujaendelea hapa mzee Patrick ana mabinti wawili hatujui mnamtaka binti gani kwahiyo wataletwa hapa mtuonyeshe, wakaletwa wasichana wawili wakiwa wamevalia khanga sare lakini pia wamejifunika sura zao wasionekane hata kuwatambua ni kazi.
mshenga: haya kijana Hawa ndo mabinti tulionao hapa nyumbani, Kama n wako kamfunue Ile nguo usoni wote tujue
Basi wote wakacheka Henry akasimama na kwenda kumfunua msichana mmoja wapo alokua amejifunika khanga, Ile kufunua akakuta sio Nissy ambaye ndo mke mtarajiwa kumbe n Martha rafiki wa Nissy akalipishwa faini ya kukosea kumtambua mtu wake, Sasa Ile kumfunua tu Humphrey alichanganyikiwa kuona Kuna dada mzuri kiasi kile...lakini akajua tu hakiharibiki kitu shemeji so ndo tunamchukua hivi.....
Basi Nissy pia akafunuliwa sura wakamuona baadae wale wasichana wakarudishwa chumbani, pale ukumbini wakaendelea kutoa mahali.Vitu Kama ng'ombe watatu,mbuzi za wajomba, suti ya baba,hela za wakina shangazi, hela kwaajili ya mama (mkaja wa mama, kwa watu wa mbeya) mablanketi,shuka,jembe na vitu kibao vilivyoorodheshwa kwenye karatasi.....Mara ujumbe mfupi unaingia kwenye Simu ya Henry "fanya utakavyoweza lakini mahali hawamalizi, kwahiyo usilipe yote" ilitoka kwa Nissy, "ni Mila tu na desturi za kabila letu eti ukimaliza wanahisi wamedharauliwa"
Henry akatabasamu tu, wakamaliza kulipa mahali kabla hawajaenda mezani mzee Mkole akamnong'oneza mzee mashaka ambaye ndo mshenga,
mzee mashaka:mh mh (akisafisha Koo na kutaka kusikilizwa) Sasa ndugu zangu tumeunganisha Koo mbili na tumekua familia moja lakini sisi tunataka kufanya harusi haraka iwezekanavyo Yani ndani ya miezi miwili tuwe tumemchukua mwali wetu....
Basi kulikua na utulivu kidogo pale ukumbini lakini ukimya ukavunjwa na familia ya mzee Patrick ambapo,
mzee Patrick:ndugu yangu naomba tusiwape jibu tujadiliane kwanza sisi Kama wanafamilia na wazazi wa Nissy. (akimwambia mshenga wao kwa sauti ya chini kidogo iliyofanya wao waelewane lakini wengine wasisikie alichokisema...
mshenga:Aiseee tunashukuru Sana na ni Jambo jema na faraja kwa wazazi lakini tunaomba tuzungumze kidogo Kama wazazi na familia ya Nissy.
mzee mashaka:hakuna shida Basi wakasogea pembeni kidogo familia yote ya Nissy na kukubaliana kitu kimoja....wakarudi Tena ukumbini.
Mshenga: Bwana Mkole na kijana wangu Hapa sisi tunaomba muongeze muda kidogo wa harusi kwakua tunajua kabisa huyu sio wetu Tena lakini Kama familia tunataka tuweze kumuaga binti yetu kwakua ametuletea heshima hapa nyumbani.
(anakunywa maji yaliyokua mezani Kisha anaendelea) muda tunaoomba ni kwaajili tu ya maandalizi na hakuna kitu kingine.
Basi familia ya mzee Mkole wakakubali na kuwaambia kuwa watakaa wapange tarehe na kuwarudishia majibu.
Basi wakakaribishwa mezani wapate chakula kilichokua kimeandaliwa.
wakiwa mezani wanaendelea Kula Henry akasikia Simu yake inaita akaitoa mfukoni akakuta ni Catty anapiga hakupokea, anaendelea Kula Simu ikapigwa zaidi ya Mara tano bila majibu na ilikua imewekwa mlio wa sauti ya chini Sana.
Mara ujumbe mfupi ukaingia "Henry kwanini hupokei Simu zangu? uko sawa kweli?"
ujumbe mwingine ukaingia "baby nimechanganyikiwa naomba ukipata ujumbe wangu unirudie hewani nimepitiliza siku kadhaa sijaona period"
****itaendelea.....
Comments
Post a Comment