NAHISI NINA MIMBA YAKO
Muda wote Henry alikua ni mtu mwenye furaha na anatabasamu lakini baada ya kupokea ujumbe mfupi kutoka kwa catty tabasamu likatoweka usoni.Basi Kwasababu ilikua ni chakula Cha pamoja kwa familia kulikua na stori nyingi za hapa na pale. Humphrey hakuelewa kinachoendelea kwa rafiki yake Basi akawa anamtania tu Humphrey: kwahiyo mwanangu Kama utani unachukua jiko, Henry: we si unataka uzeeke ngoja watu wazima tukuonyeshe njia ya kupita, Humphrey:Sema Nini mwanangu nahisi ntawahi kuoa, na tutaongea Kuna suala muhimu mno. Basi wakatawanyika kila mtu na safari yake, mzee Mkole, Henry pamoja na Humphrey walikua na safar ya kurudi Dar es salaam.wakati baba yake mdogo Henry yeye anaishi mbeya akifanya biashara zake na ni mtu aliefanikiwa katka biashara zake. Baada ya kuondoka pale walielekea kwa baba ake mdogo Henry ili walale siku hiyo kesho yake waanze safari.Baba ake mkubwa pamoja na shangazi ake Henry ambaye ni aunt Maya wao walisafiri usiku kwa gari yao kuelekea Ma...